Configure HTML/JavaScript Fire & Rescue Singida Official Blog: July 2013

Monday, July 22, 2013

Fire & Rescue Singida Official Blog: Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Singida leo l...

Fire & Rescue Singida Official Blog: Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Singida leo l...: Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Singida leo limeendelea kufanya maokozi eneo la peoples singida mjini baada ya gari ya MOHAMEDI TRANS ...
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Singida leo limeendelea kufanya maokozi eneo la peoples singida mjini baada ya gari ya MOHAMEDI TRANS yenye namba za Usajili T210APK likitokea Dodoma kuelekea Mwanza na  kupata ajali eneo hilo,
Mashahidi wa Tukio hilo wamesema ni kusuka kwa Tairi ya mbele kulia ya Gari hiyo,hakuna kifo kilichotokea ila nimajeruhi kidogo ,ila kiujumla hakuna madhara makubwa.

Hapa angalia moja ya Video ya abiria waliokuwa wakisafiri na gari hiyo:
Ushauri:Kaimu kamanda Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Singida ameshauri madereva kuwa makini pindi wanapoendesha vyombo vya moto hasa wanapopakia abiria.

Wednesday, July 17, 2013

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Singida linawatangazia wananchi wote kuwa Limeanza kufanya Ukaguzi wa Kinga na Tahadhari za Moto katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Singida.
 Ukaguzi huu wa kinga na tahadhari za moto ni wa mwaka wa fedha 2013/2014,pia ukaguzi huo utaambatana na malipo ya hati za moto kulingana na Biashara au huduma ambayo mtu huyo anaitoa.
Maeneo yatakayo husika na ukaguzi huu ni pamoja na Taasisi za serikali,taasisi za watu binafsi,maeneo ya biashara yakiwemo maduka ya jumla na rejareja,hospitali,Dispensary,vituo vya mafuta,maeneo ya ujenzi(constration Areas),camps,Farming/Grazing,Fire equipment dealer,Forestry/Logs,Gas cylinder shops.Godowns,Motor vehicle/cycle,Power stations,Guest House/ Hostel na maeneo mengine mengi kama itakavyoelezwa hapa chini kwenye muongozo wa sheria ya Udhibiti ya mwaka 2007 sheria namba 14((NO.14 OF 2007)REGULATIONS
(Made under section 32))kama ambavyo itajieleza hapa chini.
    Aidha Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Zimamoto na Uokoaji aliwataka wafanya biashra na wananchi kwa ujumla kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Jeshi la Zimamoto kwa ajili ya kufanikisha zoezi hili la Ukaguzi ili kupambana na majanga mbalimbali ambayo yangeweza kutokea.
Pia Kaimu Kamanda SSF KT.Mapunda ,ameeleza faida ambazo Mkoa zitap[ata kupitia ukaguzi huu ni,kupata elimu sahihi ya Kukabiliana na majanga mbalimbali ya moto na majanga mengine kama hayo,km vile ajali mbalimbali,pia alieleza kuwa makusanyo ya maduhuli ya serikali yaleta faida kwa mkoa husika kwani mkoa utapata Asilimia 70% ya kile kilichokusanywa kwa ajili ya manunuzi ya MAGARI YA KUZIMIA MOTO,MAGARI YA KUFANYIA MAOKOZI,MAGARI YA WAGONJWA NA KUONGEZA VITUO VINGINE VYA KUZIMIA MOTO NA UOKOAJI MKOANI SINGIDA.
Hapa chini unaweza kusoma regulation(sheria hiyo udhibiti ya mwaka 2007) kwenye link kwa lugha uitakayo kwa kubonyeza hapo palikoandikwa translate kwenye blo na utachagua lugha unayo taka ili kuisoma na kuelewa sheria hiyo vizuri.
 regulation hlfu uisome linki hii hapa:http://www.sharebeast.com/ysoas34euncr.
 hapa utaisoma sheria hiyo na utaielewa.
kwa taarifa na maelekezo Waone firemarshal na assessor mkoa wa singida au wasiliana nao kupitia E-mail: zimamotosingida@yahoo.com au kwa namba 026-2503056 au 0758338875 au 0764498205

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Singida linawatangazia wananchi wote kuwa Limeanza kufanya Ukaguzi wa Kinga na Tahadhari za Moto katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Singida.
 Ukaguzi huu wa kinga na tahadhari za moto ni wa mwaka wa fedha 2013/2014,pia ukaguzi huo utaambatana na malipo ya hati za moto kulingana na Biashara au huduma ambayo mtu huyo anaitoa.
Maeneo yatakayo husika na ukaguzi huu ni pamoja na Taasisi za serikali,taasisi za watu binafsi,maeneo ya biashara yakiwemo maduka ya jumla na rejareja,hospitali,Dispensary,vituo vya mafuta,maeneo ya ujenzi(constration Areas),camps,Farming/Grazing,Fire equipment dealer,Forestry/Logs,Gas cylinder shops.Godowns,Motor vehicle/cycle,Power stations,Guest House/ Hostel na maeneo mengine mengi kama itakavyoelezwa hapa chini kwenye muongozo wa sheria ya Udhibiti ya mwaka 2007 sheria namba 14((NO.14 OF 2007)REGULATIONS
(Made under section 32))kama ambavyo itajieleza hapa chini.
    Aidha Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Zimamoto na Uokoaji aliwataka wafanya biashra na wananchi kwa ujumla kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Jeshi la Zimamoto kwa ajili ya kufanikisha zoezi hili la Ukaguzi ili kupambana na majanga mbalimbali ambayo yangeweza kutokea.
Pia Kaimu Kamanda SSF KT.Mapunda ,ameeleza faida ambazo Mkoa zitap[ata kupitia ukaguzi huu ni,kupata elimu sahihi ya Kukabiliana na majanga mbalimbali ya moto na majanga mengine kama hayo,km vile ajali mbalimbali,pia alieleza kuwa makusanyo ya maduhuli ya serikali yaleta faida kwa mkoa husika kwani mkoa utapata Asilimia 70% ya kile kilichokusanywa kwa ajili ya manunuzi ya MAGARI YA KUZIMIA MOTO,MAGARI YA KUFANYIA MAOKOZI,MAGARI YA WAGONJWA NA KUONGEZA VITUO VINGINE VYA KUZIMIA MOTO NA UOKOAJI MKOANI SINGIDA.
Hapa chini unaweza kusoma regulation(sheria hiyo udhibiti ya mwaka 2007) kwenye link kwa lugha uitakayo kwa kubonyeza hapo palikoandikwa translate kwenye blo na utachagua lugha unayo taka ili kuisoma na kuelewa sheria hiyo vizuri.
 regulation hlfu uisome linki hii hapa:http://www.4shared.com/office/tA52p9iC/NEW_FIRE_REGULLATION_2012.html hapa utaisoma sheria hiyo na utaielewa.
kwa taarifa na maelekezo Waone firemarshal na assessor mkoa wa singida au wasiliana nao kupitia email
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Singida,limeendelea kupongezwa kwa kazi nzuri ya kupambana na majanga ya moto.Moto ambao ulitokea leo huko maeneo ya Kibaoni na kuteketeza vyumba vitatu 
 Chanzo cha Moto huo kuwa ni hitafu ya umeme.Jeshi la Zimamoto lilifanikiwa kupambana na moto huo na kuokoa mali katika Nyumba hiyo.
Aidha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limetoa tahadhali ya namna ya kupambana na majanga ya moto na utoaji taarifa sahihi kwa jeshi la Zimamoto pindi majanga hayo yatokeapo.
Mwananchi mmoja akiongea na blog hii alisema."sasa Jeshi la mkoa wa Singida limeiva kwani walifika eneo la tukio mapema na mara hii maji hayajaisha mpaka wamemaliza tukio,hongera sana Zimamoto"alimaliza kwa kusema hayo.
Pia mtoto wa mwenye nyumba hiyo ambae ni MARIAM ISSA MTATURU ameelezea tukio hilo kuwa liliwashtua sana na wamelishukuru Jeshi la Zimamoto Mkoa kwa Kuwasaidia.

HAPA CHINI NI VIDEO NA PICHA

ZA TUKIO ZIMA LA MOTO HUO HUKO KIBAONI MKOANI SINGIDA !!

 Kwa Dharula ya majanga mbalimbali ya moto na uokoaji Piga:114,026-2503111,0752-498061 na 0753-007447.Haraka kwa Msaada.

Posted by:Hassan J.Mtengevu(Afisa Habari na mawasiliano kwa Umma Mkoa wa Singida ,Jeshi la Zimamoto na Uokoaji )

Wednesday, July 3, 2013

JESHI LA ZIMAMOTO MKOA WA SINGIDA

ANGALIA VIDEO HAPA:
VIDEO :HALI YA GARI MARA BAADA MOTO HUO KUZIMWA.

DEREVA WA GARI HIYO AKIELEZEA TUKIO HILO LILIVYOTOKEA

Jeshi la zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Singida limefanikiwa kuokoa gari namba T 154 AYC Inayomilikiwa na Bw Issac Bwire wa Dar es salaam lilokuwa likiendeshwa na Dereva Allan Patric Lililokuwa Liliteketea kwa moto eneo maarufu kwa jina la kona ya Mohamedi Mjini Singida majira ya 10:55 alfajiri, Ni kama km 7 kutoka Singida Mjini,Kikosi cha zimamoto na uokoaji kilifika eneo la tukio majira ya saa 11:05 alfajiri na kuanza kuzima moto huo unaosadikiwa kuwa chanzo chake ni shoti ya umeme kwenye gari hiyo,Hata hivyo kilifanikiwa kuzima moto huo mara moja.
aidha kikosi cha zimamoto kikiongozwa na kamanda wake SSF KT.MAPUNDA walifanikiwa kuzima moto huo na kuokoa mali iliyosalia kwenye gari hiyo kama utakavyoiona kwenye video,
Hata hivyo kamanda Mapunda bado alisisiza umuhimu wa magari kutembea na vizimio vya moto mara majanga ya moto yatakapotokea uanze kukabiliana nao kabla haujaleta hasara kubwa.
Hata hivyo bado tahadhari zaidi inatakiwa kwa watumiaji wa malori hayo kuwa na vizimio vilivyo vizima tena viweke sehemu ambazo ziko wazi zaidi ili kila mtu aweze kukifanyia kazi pindi Ajali ya moto itakapo tokea.
Askari waliofika eneo la tukio na kupambana na moto Kamanda Mapunda aliwataja kuwa SGT.Aman Kessy,Sgt.Bahat H,Salum,FC Hassan J.Mtengevu(Afisa Habari Zimamoto na uokoaji Mkoa wa Singida),FC Juma S.Farijallah na FC,Sakina I.Kitwange kwa pamoja walifanikisha kuzima moto huo.
kwa dharula yeyote ya janga la moto,ajali yeyote wasiliana na: JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MKOA KWA NAMBA 114 AU 026-2503111 MARA MOJA NA WATAKUSAIDIA HARAKA IWEZEKANAVYO .TAARIFA YA MAPEMA NDIO ITAKAYOFANYA UOKOAJI UFANYIKE KWA HARAKA SANA ,IZINGATIWE KUWA KUTOA TAARIFA MAPEMA NDIO VIZURI ZAIDI KWA KURAHISISHA KAZI YA KUPAMBANA NA JANGA HILO.