Configure HTML/JavaScript Fire & Rescue Singida Official Blog

Wednesday, July 17, 2013

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Singida,limeendelea kupongezwa kwa kazi nzuri ya kupambana na majanga ya moto.Moto ambao ulitokea leo huko maeneo ya Kibaoni na kuteketeza vyumba vitatu 
 Chanzo cha Moto huo kuwa ni hitafu ya umeme.Jeshi la Zimamoto lilifanikiwa kupambana na moto huo na kuokoa mali katika Nyumba hiyo.
Aidha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limetoa tahadhali ya namna ya kupambana na majanga ya moto na utoaji taarifa sahihi kwa jeshi la Zimamoto pindi majanga hayo yatokeapo.
Mwananchi mmoja akiongea na blog hii alisema."sasa Jeshi la mkoa wa Singida limeiva kwani walifika eneo la tukio mapema na mara hii maji hayajaisha mpaka wamemaliza tukio,hongera sana Zimamoto"alimaliza kwa kusema hayo.
Pia mtoto wa mwenye nyumba hiyo ambae ni MARIAM ISSA MTATURU ameelezea tukio hilo kuwa liliwashtua sana na wamelishukuru Jeshi la Zimamoto Mkoa kwa Kuwasaidia.

HAPA CHINI NI VIDEO NA PICHA


ZA TUKIO ZIMA LA MOTO HUO HUKO KIBAONI MKOANI SINGIDA !!

 Kwa Dharula ya majanga mbalimbali ya moto na uokoaji Piga:114,026-2503111,0752-498061 na 0753-007447.Haraka kwa Msaada.


Posted by:Hassan J.Mtengevu(Afisa Habari na mawasiliano kwa Umma Mkoa wa Singida ,Jeshi la Zimamoto na Uokoaji )

1 comment:

  1. HAYA WATANZANIA TOENI MAONI YENU JUU YA HII KAZI NZURI ILIYOFANYWA NA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MKOA WA SINGIDA

    ReplyDelete