Configure HTML/JavaScript Fire & Rescue Singida Official Blog: 2013

Monday, December 2, 2013

UKAGUZI WA KINGA NA TAHADHARI ZA MOTO.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Singida linawatangazia wananchi wote kuwa Limeanza kufanya Ukaguzi wa Kinga na Tahadhari za Moto katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Singida.
 Ukaguzi huu wa kinga na tahadhari za moto ni wa mwaka wa fedha 2013/2014,pia ukaguzi huo utaambatana na malipo ya hati za moto kulingana na Biashara au huduma ambayo mtu huyo anaitoa.
Maeneo yatakayo husika na ukaguzi huu ni pamoja na Taasisi za serikali,taasisi za watu binafsi,maeneo ya biashara yakiwemo maduka ya jumla na rejareja,hospitali,Dispensary,vituo vya mafuta,maeneo ya ujenzi(constration Areas),camps,Farming/Grazing,Fire equipment dealer,Forestry/Logs,Gas cylinder shops.Godowns,Motor vehicle/cycle,Power stations,Guest House/ Hostel na maeneo mengine mengi kama itakavyoelezwa hapa chini kwenye muongozo wa sheria ya Udhibiti ya mwaka 2007 sheria namba 14((NO.14 OF 2007)REGULATIONS
(Made under section 32))kama ambavyo itajieleza hapa chini.
    Aidha Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Zimamoto na Uokoaji aliwataka wafanya biashra na wananchi kwa ujumla kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Jeshi la Zimamoto kwa ajili ya kufanikisha zoezi hili la Ukaguzi ili kupambana na majanga mbalimbali ambayo yangeweza kutokea.
Pia Kaimu Kamanda SSF KT.Mapunda ,ameeleza faida ambazo Mkoa zitapata kupitia ukaguzi huu ni,kupata elimu sahihi ya Kukabiliana na majanga mbalimbali ya moto na majanga mengine kama hayo,km vile ajali mbalimbali,pia alieleza kuwa makusanyo ya maduhuli ya serikali yalete faida kwa mkoa husika kwani mkoa utapata Asilimia 70% ya kile kilichokusanywa kwa ajili ya manunuzi ya MAGARI YA KUZIMIA MOTO,MAGARI YA KUFANYIA MAOKOZI,MAGARI YA WAGONJWA NA KUONGEZA VITUO VINGINE VYA KUZIMIA MOTO NA UOKOAJI MKOANI SINGIDA.
Hapa chini unaweza kusoma regulation(sheria hiyo udhibiti ya mwaka 2007) kwenye link kwa lugha uitakayo kwa kubonyeza hapo palikoandikwa translate kwenye blo na utachagua lugha unayo taka ili kuisoma na kuelewa sheria hiyo vizuri.




Thursday, October 17, 2013

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MKOA WA MANYARA

 JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MKOANI MANYARA LAENDELEA NA KAZI NZURI YA KUOKOA MAISHA NA MALI.


 Askari wa Jeshi la Zimamoto wakifanya uokoaji
 Gari ya zimamoto ikielekea eneo la tukio
 baadhi ya vyumba ambayo vilifanikiwa kuokolewa

Jana majira ya saa 2 usiku ,tulipokea taarifa ya tukio la moto kupitia namba yetu ya dharula 114,wakati tunatoka kituoni tulikutana na wenye pikipiki wakitufuata,haikuchukua zaidi ya dk 1 kuwasili kwenye eneo la tukio,tulipofika tulikuta moto mkubwa ukiwa juu ya paa na ukitokea madirishani,tulitumia maji tuliyoenda nayo yakaisha,tukafuata mengine yakaisha,tukafuta mengine ziwa Babati ( chanzo pekee cha kupata maji) tukakwama kidogo kwani pump ya kunyonya maji iliingia upepo,baada ya kufanikiwa kutoa upepo turudi eneo la tukio na kupooza mitungi ya gesi ya kupikia iliyokuwa bado haijalipuka na kuhakikisha moto hausambai kwenye nyumba za jirani.ilipofika saa 7 usiku zoezi la uzimaji lilikuwa limekamilika japo waathirika wapatao kumi na moja mali zao ziliteketea kwa moto.

Changamoto zetu hapa Babati ni:
1.Kutokuwa na tahadhari na kinga ya moto
2.Kuchelewa kutoa taarifa za moto
3.Kuingiliwa na wananchi (kwa nia njema ya kuokoa) kwenye shughuli ya uzimaji moto
4.Kukosa visima maalum vya kuchotea maji(fire hydrants)
5.Upungufu wa magari ya kuzimamoto
Pamoja na changamoto hizo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Manyara linaendelea kufanya vizuri katika majanga mbalimbali tena kwa weledi mkubwa.
wananchi mnaombwa mtoe taarifa kwa wakati kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ili kufanikisha mapema zoezi la uzimaji moto na uokoaji kwa wakati,vilevile kwenywe majanga mbalimbali ya Uokoaji Taarifa zifike mapema kituoni.
HII TAARIFA NI KWA HISANI YA KAMANDA WA MKOA MANYARA(RFO)

Saturday, August 10, 2013

TANZIA

OFISI YA KAMISHINA JENERALI,JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI TANZANIA,INASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA ASKARI MRAKIBU MSAIDIZI AFANDE JAFARI MOHAMEDI MADILUKA ALIYEKUWA KAIMU KAMANDA WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MKOA WA KATAVI,KILICHOTOKEA TAREHE 05/08/2013 KWA AJALI YA GARI HUKO SUMBAWANGA.

INNALILLAH WA INNA ILAHIR RAJIUN.
MAZISHI YA ALIYEKUWA KAIMU KAMANDA WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MKOA WA KATAVI,MRAKIBU MSAIDIZI  JAFARI MOHAMEDI MADILUKA,YALIYOFANYIKA KATIKA KATA YA MZUMBE WILAYA YA MVOMERO AGOSTI 8 MWAKA HUU.
Baadhi ya maofisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakibeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa kaimu kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa katavi,Mrakibu Msaidizi Jafari Mohamedi Madiluka mara baada ya kufikishwa kijijini kwake Mkongeni,kata ya Mzumbe,Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro.
Afande Madiluka alifariki kwa ajali ya gari Agost 5 mwaka huu Wilayani Sumbawanga wakati akielekea Mkoani Katavi akitokea Jijini Dar es salaam,Mazishi yamefanyika Agost 8,mwaka huu huko kijini kwake Mikongeni.
Mwili wa Afande Mohamedi ukiswaliwa tayari kwenda kuzikwa.


Kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro,Faustine Shilongile akiweka udongo kaburini.



Luten kanali ,Lidwino Simioni Mgumba,Naibu kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania,Agosti 8 mwaka huu akiweka udogo ndani ya kaburi alipozikwa afande Mohamedi.


Taratibu za mazishi ya Kiislamu zikiendelea.


Maofisa wa ngazi za juu wa Jeshi la Ziamoto na Uokaji pamoja na Majeshi mengine,wakitoa saluti ya heshima ya mwisho mara baada ya kukamilika kwa mazishi hayo.
Askari wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji wakitoa heshima kijeshi katika mazishi hayo.
Baadhi ya waombolezaji wa msiba huo waliopata bahati ya kwenda morogoro kwa mazishi,pia baadhi ya maofisa A/Inp.Taki,
Dua za kumuombea marehemu Afande Mohamedi madiluka zikiendelea,
   Mwenyezi mungu aiweke roho ya marehemu Afande Mohamedi madiluka mahali pema peponi AMIN


"HAKIKA SISI NI WA MWENYEZI MUNGU NA KWAKE TUTAREJEA"




PICHA NI KWA MSAADA WA JOHN NDITI.

Thursday, August 8, 2013

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Singida yaendelea na FATIKI ya kutengeneza na kurekebisha maeneo ya kambi yao iliyopo karakana -Singida Mjini.
Moja wapo ya jambo ambalo limenivutia ni ubunifu wa kuweka Nembo ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji chini ya ardhi eneo la wazi,Kwa kufanya ubunifu kama huu wanastyle pongezi .
Hata hivyo hapa wameonesha hisia zao na mapenzi juu ya Jeshi lao la Zimamoto na Uokoaji.
Karibu Kwenye kambi ya Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Singida Uone majabun zaidi ya kiubunifu.
 Askari Badi Mingange akiendelea na Zoezi la kulinganisha kingo za maneno hayo(JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI)(SQUARE)
 Hapa ni baadhi la maneno yanayokamilisha neno JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI ,yakiwa katika maandalizi ya mwisho tayari kupakwa rangi.

Sgt Bahati akitoa baadhi ya maelekezo ya namna gani wafanye ili kuboresha muonekano wa Neno hilo hapo chini.
HAPA ANGALIA VIDEO JINSI ZOEZI HILO LILIVYOENDESHWA:










Haya mwanchi toa maoni yako juu ya hili
walilofanya Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoa wa Singida.

Tuesday, August 6, 2013

Jeshi la Zimamoto na uokoaji Mkoa wa Singida linaendelea na kazi nzuri ya kufanya maokozi katika Mkoa wa Singida,leo tulipokea taarifa ya kutumbukia kwa mtoto kwenye kisima huko Sabasaba Maeneo ya Uwanja wa ndege Mkoa wa Singida kuwa kuna mtoto ametumbukia kwenye kisima.
Ama chanzo cha habari kinasema mtoto mdogo huyo mwenye umri wa miaka(3) alitumbukia kwenye kisima hicho akijaribu kuchota maji na kopo dogo ambalo lilikuwa maeneo hayo,kwa bahati mbaya akatumbukia kwenye shimo hilo na kusababishia umauti.
Aidha Jeshi la Zimamoto lilipopatiwa taarifa hizi leo mara moja wakiongozwa na Kamanda wa Mkoa SSF.KT.MAPUNDA walifika eneo la tukio kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi walichukua maiti hiyo na kwenda nayo hospitali kwa uchunguzi zaidi.
USHAURI:Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa aliwashauri wananchi kuwa makini na watoto wadogo na vitu vya hatari kama visima na maeneo mengine,vilevile alishauri kupandisha kuta za kisima hicho kwa kuepuka majanga zaidi,pia kuwashauri wananchi kutoa taarifa mapema zaidi kwa Jeshi la Zimamoto kwa Msaada Zaidi wa Haraka,
Piga namba:114/0752-498061/0767-051147/0753-007447 kwa msaada wa haraka pindi majanga yatokeapo.
 Gari ya Polisi iliyobeba mwili wa marehemu kuelekea hospitali ya Mkoa wa Singida kwa Uchunguzi.
 Sgt.Bahati wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji akifanya mahojiano na baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo.
 Hiki ndicho kisima kilichochukua uhai wa huyo Mtoto.
 Mahojiano yakiendelea
 Maiti ikiwa kwenye gari ya Polisi tayari kwenda Hospitali ya Mkoa.
Kamanda wa Mkoa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji SSF KT.MAPUNDA akitoa maelekezo na ushauri ,pia alitoa pole kwa wafiwa wa Msiba huo.
video ya Afisa usalama akitoa maelezo juu ya Tukio hilo.

Friday, August 2, 2013

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Singida,limeendelea na Zoezi la Ukaguzi sehemu mbalimabli za Mkoa.
Jeshi la zimamoto limeanza ukaguzi huo maeneo ya serikali,maeneo hayo ni pamoja na VETA -SINGIDA,CHUO CHA WASIOONA,IDARA YA MAJI-MANISPAA(SUWASA)NA TBA(WAKALA WA MAJENGO).
Kupitia ukaguzi huo imekutana na changamoto mbalimbali kama wahusika kutokuwa na uelewa juu ya kinga na tahadhari za moto na majanga mbalimbali.
VETA -SINGIDA,
Hapa tulikutana na changamoto kidogo tu kama vile vifaa vya kuzimia moto vilikuwa havijafanyiwa matengezo hata hivyo mkuu wa chuo alituhakikishia kufanyiwa service haraka,hii ni pamoja na kumpigia simu wakala na kweli alikuja na kuanza kuzifanyia matengenezo,katika hili VETA SINGIDA tunawapongeza sana.
Hapa angalia picha za wakaguzi wa Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Singida wakifanya ukaguzi.

 Hapa ni Jengo la utawala VETA-SINGIDA mara baada ya ukaguzi.
 Askari Ansgar Ngaromba akikagua mitungi katika Jengo la utawala
 Askari Sakina Akikagua baadhi ya machine katika kitengo cha ufundi Bomba
 Wakaguzi wa Jeshi la Zimamoto wakimpa maelekezo Mwl.Triphone Maricel kitengo cha Ufundi Umeme Veta-Singida.
picha hapo juu ni mwl wa ushonaji Veta Singida akipewa maelekezo na Askari Ngaromba.
Aidha mara baada ya ukaguzi huo,ambao tulifanya tukiongozwa na Afisa Ununuzi na Ugavi Veta Singida Bw.Eliah.A.Eliah,Alieleza changamoto mbalimali kwa jeshi la zimamoto na pia alitoa shukrani kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa kwa Ukaguzi huo,kwa niaba ya Mkuu wa Chuo hicho.
HAPA ANGALIA VIDEO YA MAELEZO YA AFISA HUYO WA UGAVI.
Ukaguzi uliendelea kwa kutembelea Chuo cha wasioona Singida.
Hapo tulikutana na kaimu mkuu wa Chuo hicho,Mwl.Moyo nae alituonesha ushirikiano wa kutosha kufanikisha zoezi letu la ukaguzi.
Mwalimu Moyo alisema Chuo kna aina mbili za Wanafunzi,
  1. Walemavu
  2. Wasio na Ulemavu.
chuo kiujumla kina wanafunzi 160 lakini kwa sasa  wanafunzi 42 wamekwenda Field kwa mazoezi ya Vitendo,hapa angalia jinsi ukaguzi huo ulivyofanyika na Jeshi la zimamoto limegundua mapungu mengi katika Chuo hiki.
moja ya mapungufu hayo ni: Chuo chote hakina kizimio cha moto hata kimoja,wanafunzi wa bweni wanalala wengi,madirisha madogo,switch za umeme ziko vibaya waya ziko nje,na hii ni hatari na inaweza leta majanga ya moto katika chuo hicho.
PICHA:
 Askari wa Jeshi la zimamoto na Uokoaji wakiendelea na Ukaguzi katika Chuo hicho.
 Wanafunzi wa Chuo hicho cha wasioona wakiwa darasani.
 Mfumo mbaya wa ungaji wa waya za umeme katika chuo hicho ambao unaweza kuleta majanga ya moto katika Chuo hicho.
 Mrundikano wa wanafunzi, katika chumba kimoja kuna wanafunzi 8,na chumba hicho ni kidogo sana madirisha madogo mno,walishauriwa na Mtathmini Boniface wapunguze idadi ya wanafunzi kwenye mabweni hadi kufikia wanafunzi wanne.
 Hii ndio hali ya mabweni hayo kama yanavyoona
hii ndio hali ya uunganishwaji wa kiholela wa waya za umeme kwenye chuo hicho.
Aidha Jeshi la Zimamoto na uokoaji liligundua mapupungu yafuatayo katika chuo hicho:
  1. Mfumo mbaya wa umeme,
  2. Msongamano wa vitanda na wanafunzi kwenye mabweni.
  3. Baadhi ya vitanda havina ngazi ya kupandia
  4. Wamepaka rangi za mafuta kuta zote za Chuo hicho
  5. Hakuna kizimio hata kimoja.
Firemarshall alitoa ushauri wa kitaalamu juu ya mapungufu hayo.
Angalia video ya Kaimu mkuu wa Chuo:

 Baada ya hapo ukaguzi uliendelea kwa kukagua ofisi za Idara ya Maji manispaa ya Singida(SUWASA).
Hapa tulipokelewa na Afisa Utawala na Rasilimali watu wa Idara ya maji,Bi Fatina Amiri Mbaga,ambae alituonesha ushirikiano wa kutosha kuzunguka sehemu mbalimbali za ofisi hiyo ya idara ya maji manispaa ya singida.
Hata hivyo nao pia tulikuta mapungufu mbalimbali yakiwemo ya:
  1. Mfumo mbaya wa umeme
  2. Mitungi hakuna
  3. Ofisi ya Afisa mahusiano kuna nyufa chini na ukutani
  4. Mpangilio mbaya wa vifaa vya stoo ambao ni hatari.
  5. Upakaji wa rangi za mafuta katika ofisi zao.
hapa angalia Askari wakifanya ukaguzi katika ofisi hizo:
 mmoja ya mpangilio mbaya wa vifaa katika moja ya ofisi za SUWASA-Singida mjini.
Eneo la juu ya paa kwa ndani kumeharibika vibaya na kufanya eneo hilo la korido kuwa hatari kwa watumishi wa ofisi hiyo.
Mojawapo ya stoo zao za ununuzi na ugavi za Suwasa na namna mpangilio wao ulivyokuwa mbaya.
Hii ni stoo ya mabomba ya maji na mpangilio wao mbaya wa vifaa hivi
moja ya maghala ya mafundi wa SUWASA -SINGIDA
Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Singida wakiendelea na Ukaguzi katika moja ya stoo za SUWASA.


Hata hivyo tulipokamilisha ukaguzi katika Ofisi hizo za SUWASA ,aAfisa utawala na Rasilimali watu alikuwa na Haya ya Kusema:
Video:
Ama baada ya hapo jeshi la Zimamoto likaendelea na ukaguzi  na sasa tukaingia ofisi za TBA Wakala wa majengo
Halikadhalika tulikaribishwa vizuri ofisi ya TBA Mkoa na tulikaribishwa na mwakilishi wa Meneja wa Mkoa Bw.Mohamedi Soloka yeye ni Estate Officer Majengo na Usanifu Mkoa.
Hapa pia tulikutana na mapungufu mengi tu,moja ya mapungufu hayo ni pamoja na :
  1. Hakuna mitungi ya kuzimia moto
  2. Mpangilio wa vifaa vya stoo ni mbovu kabisa
  3. Sakafu zimepasuka eneo la carteen ya Ofisi
  4. Mfumo wa umeme sio mzuri
Analia baadhi ya picha za Ofisi hiyo ya TBA Mkoa wa singida.
Hii ni Ofisi ya Mhasibu mkoa wa TBA  N a ndio huyo hapo anaeonekana hapo.
kama unavyoona mpangilio wa mafaili kwa Mhasibu huyo wa Mkoa wa TBA.
Hii ni moja ya stoo zao na mpangilo wao mbaya kama unavyoonekana.


Hii ni ofisi ya Bw.Mohamedi Soloka ambae ni Msanifu na Majengo Mkoa wa TBA.

HAPA ANGALIA VIDEO YA MAHOJIANO KATI YA AFISA HABARI NA MAWASILIANO KWA UMMA WA JESHI LA ZIMAMOTO ASKARI HASSAN MTENGEVU NA BW.SOLOKA MSANIFU NA MAJENGO WA TBA-MKOA


Aidha baada ya hapoFiremarshall alitoa ushauri wa kitaalamu juu ya mapungufu hayo.Ukaguzi bado unaendelea katika maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Singida,na elimu kwa umma pia inaendelea kupitia njia mbali mbali,kama vipeperushi ,mitandao ya kijamii na mabango mbalimbali hapa mkoani.