Configure HTML/JavaScript Fire & Rescue Singida Official Blog: December 2013

Monday, December 2, 2013

UKAGUZI WA KINGA NA TAHADHARI ZA MOTO.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Singida linawatangazia wananchi wote kuwa Limeanza kufanya Ukaguzi wa Kinga na Tahadhari za Moto katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Singida.
 Ukaguzi huu wa kinga na tahadhari za moto ni wa mwaka wa fedha 2013/2014,pia ukaguzi huo utaambatana na malipo ya hati za moto kulingana na Biashara au huduma ambayo mtu huyo anaitoa.
Maeneo yatakayo husika na ukaguzi huu ni pamoja na Taasisi za serikali,taasisi za watu binafsi,maeneo ya biashara yakiwemo maduka ya jumla na rejareja,hospitali,Dispensary,vituo vya mafuta,maeneo ya ujenzi(constration Areas),camps,Farming/Grazing,Fire equipment dealer,Forestry/Logs,Gas cylinder shops.Godowns,Motor vehicle/cycle,Power stations,Guest House/ Hostel na maeneo mengine mengi kama itakavyoelezwa hapa chini kwenye muongozo wa sheria ya Udhibiti ya mwaka 2007 sheria namba 14((NO.14 OF 2007)REGULATIONS
(Made under section 32))kama ambavyo itajieleza hapa chini.
    Aidha Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Zimamoto na Uokoaji aliwataka wafanya biashra na wananchi kwa ujumla kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Jeshi la Zimamoto kwa ajili ya kufanikisha zoezi hili la Ukaguzi ili kupambana na majanga mbalimbali ambayo yangeweza kutokea.
Pia Kaimu Kamanda SSF KT.Mapunda ,ameeleza faida ambazo Mkoa zitapata kupitia ukaguzi huu ni,kupata elimu sahihi ya Kukabiliana na majanga mbalimbali ya moto na majanga mengine kama hayo,km vile ajali mbalimbali,pia alieleza kuwa makusanyo ya maduhuli ya serikali yalete faida kwa mkoa husika kwani mkoa utapata Asilimia 70% ya kile kilichokusanywa kwa ajili ya manunuzi ya MAGARI YA KUZIMIA MOTO,MAGARI YA KUFANYIA MAOKOZI,MAGARI YA WAGONJWA NA KUONGEZA VITUO VINGINE VYA KUZIMIA MOTO NA UOKOAJI MKOANI SINGIDA.
Hapa chini unaweza kusoma regulation(sheria hiyo udhibiti ya mwaka 2007) kwenye link kwa lugha uitakayo kwa kubonyeza hapo palikoandikwa translate kwenye blo na utachagua lugha unayo taka ili kuisoma na kuelewa sheria hiyo vizuri.