TANZIA
OFISI YA KAMISHINA JENERALI,JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI TANZANIA,INASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA ASKARI MRAKIBU MSAIDIZI AFANDE JAFARI MOHAMEDI MADILUKA ALIYEKUWA KAIMU KAMANDA WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MKOA WA KATAVI,KILICHOTOKEA TAREHE 05/08/2013 KWA AJALI YA GARI HUKO SUMBAWANGA.
MAZISHI YA ALIYEKUWA KAIMU KAMANDA WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MKOA WA KATAVI,MRAKIBU MSAIDIZI JAFARI MOHAMEDI MADILUKA,YALIYOFANYIKA KATIKA KATA YA MZUMBE WILAYA YA MVOMERO AGOSTI 8 MWAKA HUU.INNALILLAH WA INNA ILAHIR RAJIUN.
Baadhi ya maofisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakibeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa kaimu kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa katavi,Mrakibu Msaidizi Jafari Mohamedi Madiluka mara baada ya kufikishwa kijijini kwake Mkongeni,kata ya Mzumbe,Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro.
Afande Madiluka alifariki kwa ajali ya gari Agost 5 mwaka huu Wilayani Sumbawanga wakati akielekea Mkoani Katavi akitokea Jijini Dar es salaam,Mazishi yamefanyika Agost 8,mwaka huu huko kijini kwake Mikongeni.
Mwili wa Afande Mohamedi ukiswaliwa tayari kwenda kuzikwa.
Luten kanali ,Lidwino Simioni Mgumba,Naibu kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania,Agosti 8 mwaka huu akiweka udogo ndani ya kaburi alipozikwa afande Mohamedi.
Taratibu za mazishi ya Kiislamu zikiendelea.
Maofisa wa ngazi za juu wa Jeshi la Ziamoto na Uokaji pamoja na Majeshi mengine,wakitoa saluti ya heshima ya mwisho mara baada ya kukamilika kwa mazishi hayo.
Askari wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji wakitoa heshima kijeshi katika mazishi hayo.
Baadhi ya waombolezaji wa msiba huo waliopata bahati ya kwenda morogoro kwa mazishi,pia baadhi ya maofisa A/Inp.Taki,
Dua za kumuombea marehemu Afande Mohamedi madiluka zikiendelea,
Mwenyezi mungu aiweke roho ya marehemu Afande Mohamedi madiluka mahali pema peponi AMIN
"HAKIKA SISI NI WA MWENYEZI MUNGU NA KWAKE TUTAREJEA"
PICHA NI KWA MSAADA WA JOHN NDITI.
No comments:
Post a Comment