Configure HTML/JavaScript Fire & Rescue Singida Official Blog

Tuesday, August 6, 2013

Jeshi la Zimamoto na uokoaji Mkoa wa Singida linaendelea na kazi nzuri ya kufanya maokozi katika Mkoa wa Singida,leo tulipokea taarifa ya kutumbukia kwa mtoto kwenye kisima huko Sabasaba Maeneo ya Uwanja wa ndege Mkoa wa Singida kuwa kuna mtoto ametumbukia kwenye kisima.
Ama chanzo cha habari kinasema mtoto mdogo huyo mwenye umri wa miaka(3) alitumbukia kwenye kisima hicho akijaribu kuchota maji na kopo dogo ambalo lilikuwa maeneo hayo,kwa bahati mbaya akatumbukia kwenye shimo hilo na kusababishia umauti.
Aidha Jeshi la Zimamoto lilipopatiwa taarifa hizi leo mara moja wakiongozwa na Kamanda wa Mkoa SSF.KT.MAPUNDA walifika eneo la tukio kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi walichukua maiti hiyo na kwenda nayo hospitali kwa uchunguzi zaidi.
USHAURI:Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa aliwashauri wananchi kuwa makini na watoto wadogo na vitu vya hatari kama visima na maeneo mengine,vilevile alishauri kupandisha kuta za kisima hicho kwa kuepuka majanga zaidi,pia kuwashauri wananchi kutoa taarifa mapema zaidi kwa Jeshi la Zimamoto kwa Msaada Zaidi wa Haraka,
Piga namba:114/0752-498061/0767-051147/0753-007447 kwa msaada wa haraka pindi majanga yatokeapo.
 Gari ya Polisi iliyobeba mwili wa marehemu kuelekea hospitali ya Mkoa wa Singida kwa Uchunguzi.
 Sgt.Bahati wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji akifanya mahojiano na baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo.
 Hiki ndicho kisima kilichochukua uhai wa huyo Mtoto.
 Mahojiano yakiendelea
 Maiti ikiwa kwenye gari ya Polisi tayari kwenda Hospitali ya Mkoa.
Kamanda wa Mkoa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji SSF KT.MAPUNDA akitoa maelekezo na ushauri ,pia alitoa pole kwa wafiwa wa Msiba huo.
video ya Afisa usalama akitoa maelezo juu ya Tukio hilo.

No comments:

Post a Comment