Configure HTML/JavaScript Fire & Rescue Singida Official Blog: July 2016

Thursday, July 28, 2016

UCHANGIAJI WA DAMU KUOKOA MAISHA

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania inaungana na watu wengine kushiriki katika kampeni ya uchangiaji Damu wa hiari kwani Uchangiaji wa Damu ni Zawadi ya maisha.
NANI ANASTAHILI KUCHANGIA DAMU:-
  • Mtu yeyote mwenye umri kati ya 18 hadi 65.
  • Mwenye uzito usiopungua kilo 65
  • Awe na Afya Njema.
FAIDA ZA KUCHANGIA DAMU:
Kuchangia Damu ni Kuokoa maisha ya Mtu mmoja au zaidi,na hii ni Zawadi kubwa ambayo binadamu anaweza kuumpa binadamu mwenzie.
    Imeelezwa kuwa kuchangia Damu mwanamke anaweza kuchangia mara tatu(03) kwa Mwaka na mwanaume anaweza kuchangia mara nne(04) kwa Mwaka.
Kwa kawaida mwili wa mwanadamu una damu galoni tano(05) hadi saba(07), na kwa kawaida unapochangia Damu kiasi cha Mililita 450 kinachotolewa.Mchangiaji hubaki na kiasi cha kutosha cha Damu hakuna haja ya kuwa na hofu.
MUHIMU:
                 Mtu yeyote mwenya magonjwa ya kurith haruhusiwi kuchangia damu.



UCHANGIAJI WA DAMU NI ZAWADI YA MAISHA NA UTAPATA THAWABU KWA MUNGU-Na Sgt H.J Mtengevu Kaimu Afisa Habari na Elimu kwa Umma Mkoa wa Singida.

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

Tatizo la majanga ya moto kwenye Jamii kutodhibitiwa kwa wakati au mapema..................Wanaochangia hili ni wananchi wenyewe kwa kiasi kikubwa kwa sehemu ndogo sana lawama tunaweza peleka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwamaana hatutoi taarifa kwa wakati kwa Jeshi la Zimamoto.JADILI!!!!!!!!!!!!! Na Sgt H.J.Mtengevu-Kaimu Afisa Habari na Elimu kwa Umma Mkoa wa Singida.