Configure HTML/JavaScript Fire & Rescue Singida Official Blog: JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MKOA WA MANYARA

Thursday, October 17, 2013

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MKOA WA MANYARA

 JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MKOANI MANYARA LAENDELEA NA KAZI NZURI YA KUOKOA MAISHA NA MALI.


 Askari wa Jeshi la Zimamoto wakifanya uokoaji
 Gari ya zimamoto ikielekea eneo la tukio
 baadhi ya vyumba ambayo vilifanikiwa kuokolewa

Jana majira ya saa 2 usiku ,tulipokea taarifa ya tukio la moto kupitia namba yetu ya dharula 114,wakati tunatoka kituoni tulikutana na wenye pikipiki wakitufuata,haikuchukua zaidi ya dk 1 kuwasili kwenye eneo la tukio,tulipofika tulikuta moto mkubwa ukiwa juu ya paa na ukitokea madirishani,tulitumia maji tuliyoenda nayo yakaisha,tukafuata mengine yakaisha,tukafuta mengine ziwa Babati ( chanzo pekee cha kupata maji) tukakwama kidogo kwani pump ya kunyonya maji iliingia upepo,baada ya kufanikiwa kutoa upepo turudi eneo la tukio na kupooza mitungi ya gesi ya kupikia iliyokuwa bado haijalipuka na kuhakikisha moto hausambai kwenye nyumba za jirani.ilipofika saa 7 usiku zoezi la uzimaji lilikuwa limekamilika japo waathirika wapatao kumi na moja mali zao ziliteketea kwa moto.

Changamoto zetu hapa Babati ni:
1.Kutokuwa na tahadhari na kinga ya moto
2.Kuchelewa kutoa taarifa za moto
3.Kuingiliwa na wananchi (kwa nia njema ya kuokoa) kwenye shughuli ya uzimaji moto
4.Kukosa visima maalum vya kuchotea maji(fire hydrants)
5.Upungufu wa magari ya kuzimamoto
Pamoja na changamoto hizo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Manyara linaendelea kufanya vizuri katika majanga mbalimbali tena kwa weledi mkubwa.
wananchi mnaombwa mtoe taarifa kwa wakati kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ili kufanikisha mapema zoezi la uzimaji moto na uokoaji kwa wakati,vilevile kwenywe majanga mbalimbali ya Uokoaji Taarifa zifike mapema kituoni.
HII TAARIFA NI KWA HISANI YA KAMANDA WA MKOA MANYARA(RFO)

No comments:

Post a Comment