Configure HTML/JavaScript Fire & Rescue Singida Official Blog: JESHI LA ZIMAMOTO MKOA WA SINGIDA

Wednesday, July 3, 2013

JESHI LA ZIMAMOTO MKOA WA SINGIDA

ANGALIA VIDEO HAPA:
VIDEO :HALI YA GARI MARA BAADA MOTO HUO KUZIMWA.

DEREVA WA GARI HIYO AKIELEZEA TUKIO HILO LILIVYOTOKEA



Jeshi la zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Singida limefanikiwa kuokoa gari namba T 154 AYC Inayomilikiwa na Bw Issac Bwire wa Dar es salaam lilokuwa likiendeshwa na Dereva Allan Patric Lililokuwa Liliteketea kwa moto eneo maarufu kwa jina la kona ya Mohamedi Mjini Singida majira ya 10:55 alfajiri, Ni kama km 7 kutoka Singida Mjini,Kikosi cha zimamoto na uokoaji kilifika eneo la tukio majira ya saa 11:05 alfajiri na kuanza kuzima moto huo unaosadikiwa kuwa chanzo chake ni shoti ya umeme kwenye gari hiyo,Hata hivyo kilifanikiwa kuzima moto huo mara moja.
aidha kikosi cha zimamoto kikiongozwa na kamanda wake SSF KT.MAPUNDA walifanikiwa kuzima moto huo na kuokoa mali iliyosalia kwenye gari hiyo kama utakavyoiona kwenye video,
Hata hivyo kamanda Mapunda bado alisisiza umuhimu wa magari kutembea na vizimio vya moto mara majanga ya moto yatakapotokea uanze kukabiliana nao kabla haujaleta hasara kubwa.
Hata hivyo bado tahadhari zaidi inatakiwa kwa watumiaji wa malori hayo kuwa na vizimio vilivyo vizima tena viweke sehemu ambazo ziko wazi zaidi ili kila mtu aweze kukifanyia kazi pindi Ajali ya moto itakapo tokea.
Askari waliofika eneo la tukio na kupambana na moto Kamanda Mapunda aliwataja kuwa SGT.Aman Kessy,Sgt.Bahat H,Salum,FC Hassan J.Mtengevu(Afisa Habari Zimamoto na uokoaji Mkoa wa Singida),FC Juma S.Farijallah na FC,Sakina I.Kitwange kwa pamoja walifanikisha kuzima moto huo.
kwa dharula yeyote ya janga la moto,ajali yeyote wasiliana na: JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MKOA KWA NAMBA 114 AU 026-2503111 MARA MOJA NA WATAKUSAIDIA HARAKA IWEZEKANAVYO .TAARIFA YA MAPEMA NDIO ITAKAYOFANYA UOKOAJI UFANYIKE KWA HARAKA SANA ,IZINGATIWE KUWA KUTOA TAARIFA MAPEMA NDIO VIZURI ZAIDI KWA KURAHISISHA KAZI YA KUPAMBANA NA JANGA HILO.











No comments:

Post a Comment